Jumanne 19 Mei 2026 - 22:30
Shahidi Raisi hakutambua usiku wala mchana katika kuwahudumia wananchi/ Kamwe hakusalimu amri mbele ya adui

Hawza/ Ayatullah Nouri Hamadani alisisitiza kuwa: Shahidi Raisi katika njia ya kuwahudumia wananchi hakutambua usiku wala mchana, na athari za imani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu zilikuwa dhahiri mno ndani ya nafsi yake kiasi kwamba hakuwahi kuinamisha kichwa mbele ya adui, lakini mbele ya wananchi alikuwa mnyenyekevu na msikivu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, maandishi kamili ya ujumbe wa Ayatullah Nouri Hamedani kwa mnasaba wa kufanyika kwa hafla ya mwaka wa pili tangu kuaga dunia shahidi Ayatullah Sayyid Ibrahim Raisi mjini Qum ni kama ifuatavyo:

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِیمِ

الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِینَ، وَ الصَّلَاةُ وَ السَّلَامُ عَلَی سَیِّدِنَا وَ نَبِیِّنَا أَبِی الْقَاسِمِ الْمُصْطَفَی مُحَمَّدٍ، وَ عَلَی أَهْلِ بَیْتِهِ الطَّیِّبِینَ الطَّاهِرِینَ، سِیَّمَا بَقِیَّةِ اللَّهِ فِی الْأَرَضِینَ، وَ لَعْنَةُ اللَّهِ عَلَی أَعْدَائِهِمْ أَجْمَعِینَ إِلَی یَوْمِ الدِّینِ

Natoa salamu na pongezi kwa mkusanyiko wenye heshima ambao umefanyika kutokana na mnasaba wa kumuenzi mmoja wa shakhsia zilizotoa huduma kubwa na mashuhuri za mfumo mtukufu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, yaani Hujjatul-Islam wal-Muslimin Bw. Raisi “Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake”.

Kwa ajili ya kuthamini watu katika mafundisho ya Uislamu, vigezo mbalimbali vimeainishwa, ambapo muhimu zaidi miongoni mwavyo ni kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na ikhlasi katika matendo; jambo ambalo hujitokeza katika tabia na mwenendo wa watu wenye imani, katika uga wa maisha ya kijamii pia, ibada bora zaidi ni ile inayosababisha kupatikana ridhaa ya Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Ta‘ala.

Kwa msingi huu, moja ya alama muhimu zaidi za kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu ni kuwahudumia watu; yaani mwanadamu aishi kwa namna ambayo uwepo wake uwe chanzo cha kheri na manufaa kwa waja wa Mwenyezi Mungu.

Mtume Mtukufu (saww) amesema:


“Yapo mambo mawili ambayo hakuna jema lililo juu yake: kumuamini Mwenyezi Mungu na kuwanufaisha waja wa Mwenyezi Mungu.”

Na katika kauli nyingine kutoka kwake aliulizwa ni mtu gani anayependwa zaidi na Mwenyezi Mungu Mtukufu? Akasema: «أفْضَلُ النّاسِ أنْفَعُهُم لِلنّاسِ». “Mbora wa watu ni yule mwenye manufaa zaidi kwa watu.”

Marehemu Bw. Raisii alikuwa mmoja wa nyuso ambazo katika kipindi cha uhai wake alijitahidi kwa ajili ya ridhaa ya Mwenyezi Mungu, na siku zote aliifanya ikhlasi katika matendo kuwa msingi wa kazi zake, na akajitolea nafsi yake yote kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.

Yeye katika kupita njia ngumu za huduma hakuwahi kujipa nafasi ya kuchoka, na siku zote alikuwa akiweka mbele maslahi ya Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu, katika kuwahudumia wananchi hakuutambua usiku wala mchana, athari za imani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu zilikuwa dhahiri mno ndani ya nafsi yake kiasi kwamba hakuwahi kuinamisha kichwa mbele ya adui, lakini mbele ya wananchi alikuwa mnyenyekevu na mwenye usikivu.

Katika utiifu kwa Wilayah, kushikamana na damu ya mashahidi, malengo ya Imam marehemu na kumfuata Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, hakuwahi kuwa na shaka yoyote, na hadi mwisho wa maisha yake alikuwa akijitambulisha kuwa ni mwanafunzi wa kawaida na mnyenyekevu.

Vyeo na majukumu ya kidunia hayakuwa na athari yoyote katika roho yake, na ikhlasi ileile pamoja na uchamungu vilionekana katika hatua zote za maisha yake, katika uga wa mahakama, huduma katika Haram ya Quds Razavi, na pia katika jukumu la urais, aliutumia uwezo wake wote kwa ajili ya kuinua hadhi ya nchi.

Mimi, kwa utambuzi niliokuwa nao kuhusu shakhsia hii kwa zaidi ya miaka arobaini, nashuhudia kwamba yeye katika njia ya huduma hakuacha juhudi wala kujituma kwa namna yoyote ile, na hatimaye akiwa katika hali ya kuwahudumia wananchi na katika njia ya kutekeleza wajibu alipata fadhila ya kuwa shahidi.

Kumthamini mwanadamu huyu msafi ni hatua yenye kustahiki na ipo mahali pake, ni lazima huduma zake zenye kudumu na zenye thamani zibainishwe na kuelezwa kwa wananchi.

Mwisho, ninawashukuru na kuwapongeza waandaaji wa kongamano hili, na ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape wote tawfiq.

28 Ordibehesht 1405 | 18 May 2026
Hussein Nouri Hamedani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha